Jumamosi 16 Mei 2026 - 12:30
Trump ndiye anayehusika na ukosefu wa usalama Mashariki ya Kati na kuyumba kwa utulivu katika Ghuba ya Uajemi

Hawza / Maulavi Fazlur Rahman katika hotuba yake alimwelezea Donald Trump, Rais wa Marekani, kuwa ndiye sababu kuu ya ukosefu wa usalama ndani ya Mashariki ya Kati na kuyumba kwa utulivu katika eneo la Ghuba ya Uajemi, na akasisitiza: Trump hastahili Tuzo ya Amani ya Nobel, bali ndiye anayehusika na kuunda mazingira ya kivita katika eneo hili.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Maulavi Fazlur Rahman, Rais wa Jamiat Ulema-e-Islam Pakistan, katika matamshi makali dhidi ya sera za Marekani, alimwelezea Donald Trump, Rais wa Marekani, kuwa mmoja wa sababu kuu za ukosefu wa usalama na kutokuwepo kwa utulivu ndani ya Mashariki ya Kati na eneo la Ghuba ya Uajemi.

Pia huku akikosoa misimamo ya Washington dhidi ya nchi za eneo hili, alisisitiza kwamba; Trump si tu hastahili kupokea Tuzo ya Amani ya Nobel, bali utendaji wake katika miaka iliyopita umesababisha kuongezeka kwa mivutano na kuenea kwa mazingira ya vita na migogoro katika eneo hili.

Maulavi Fazlur Rahman aliendelea kusema: Inashangaza kwamba mtu ambaye kwa upande mmoja alijiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 na Iran na kuweka mazingira ya kuongezeka kwa mivutano, leo anatambulishwa kama sura ya kutaka amani.

Kwa mujibu wa kauli yake, sera ya mashinikizo, vikwazo na vitisho vya kijeshi dhidi ya Iran si tu kwamba haikusaidia amani, bali imeweka eneo hili zaidi katika hatari ya migogoro na mapambano.

Rais wa Jamiat Ulema-e-Islam Pakistan, pia huku akirejelea maendeleo ya hivi karibuni katika eneo hili alisema kwamba; Marekani sasa inajaribu kupitia mashinikizo ya kisiasa na kijeshi kuilazimisha Iran kukubali makubaliano mapya; mtazamo ambao kwa mujibu wake hautakuwa na matokeo mengine isipokuwa kuongezeka kwa kutokuaminiana na ukosefu wa usalama, na kwamba mataifa ya eneo hili yanafahamu vyema kuwa migogoro mingi ya sasa ina mizizi katika sera za Marekani za kuingilia mambo ya wengine.

Maulavi Fazlur Rahman katika sehemu nyingine ya hotuba yake pia alikosoa vikali sera za Marekani kuhusu Ghaza, na alisema kwamba; serikali ya Marekani kwa kuunga mkono kisiasa, kifedha na kijeshi utawala wa Kizayuni, ni mshirika katika mauaji ya wananchi wa Palestina.

Aliongeza kuwa: Uungaji mkono wa Washington kwa Israel umeweka mazingira ya kuendelea kwa vita na kuenea kwa mapambano katika eneo hili, na athari za mgogoro huu sasa zimefika pia katika nchi nyingine za eneo hili.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha